Resource Details
DHANA ISIYO YA KWELI:
“Fiziotherapi ni mazoezi ya mwili. Mtu anaweza kufanya mwenyewe nyumbani bila kuhitaji mtaalamu wa fiziotherapi!”
UKWELI:
Fiziotherapi si mazoezi ya kawaida tu. Ni huduma ya kitaalamu ya afya inayolenga kumsaidia mtu kurejesha, kuboresha au kudumisha uwezo wa mwili wa kufanya kazi na kushiriki katika shughuli za kila siku.
Fiziotherapi huhusisha tathmini ya hali ya mgonjwa, kubaini changamoto zinazohusiana na maumivu, mjongeo wa mwili, nguvu za misuli, usawa wa mwili, uwezo wa kutembea na utendaji wa mwili, kisha kupanga na kutoa huduma inayofaa kulingana na mahitaji ya mgonjwa