Resources & Downloads

Downloads

Visababishi vya PID na madhara yake PDF

Visababishi vya PID na madhara yake

Ugonjwa wa Maambukizi ya Via vya Uzazi vya Ndani ya Nyonga (Pelvic Inflammatory Disease – PID) ni tatizo muhimu la afya ya uzazi linaloathiri viungo vya uzazi vya mwanamke, ikiwemo mfuko wa uzazi, mirija ya uzazi na wakati mwingine ovari. Chapisho hili la kielimu lililoandaliwa na Rally Polyclinic na kuandikwa na Dkt. Leonard Cornel linaelezea visababishi, dalili, njia za uchunguzi, matibabu na madhara yanayoweza kusababishwa na PID. Kupitia maswali na majibu kumi, chapisho hili linajibu maswali yanayoulizwa mara kwa mara, linaondoa dhana potofu na kutoa elimu kuhusu namna ya kujikinga. Pia, linasisitiza umuhimu wa kutambua ugonjwa mapema na kupata matibabu sahihi ili kuzuia madhara makubwa kama vile ugumba, mimba kutunga nje ya kizazi na maumivu sugu ya nyonga. Lengo kuu ni kuongeza uelewa wa jamii, kuhamasisha upimaji na matibabu kwa wakati na kulinda afya ya uzazi wa mwanamke.

355.44 KB
View Details
Madhara ya uvaaji wa viatu vya visigino virefu PDF

Madhara ya uvaaji wa viatu vya visigino virefu

Viatu virefu ni sehemu ya mitindo ya uvaaji inayopendwa na watu wengi kwa sababu huongeza mvuto na kujiamini. Hata hivyo, je, umewahi kujiuliza ni kwa kiasi gani matumizi ya viatu virefu yanaweza kuathiri afya ya miguu na sehemu nyingine za mwili? Kuvaa viatu virefu mara kwa mara, hasa kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo kwenye sehemu ya mbele ya unyayo, kuathiri usawa wa mwili na kubadilisha namna tunavyotembea. Hali hii inaweza kuchangia maumivu ya nyayo, vifundo vya miguu, magoti, nyonga na mgongo, pamoja na kuongeza hatari ya kujikwaa au kuanguka. Athari hutegemea urefu na muundo wa kiatu, muda wa matumizi na hali ya afya ya mtu. Kupitia uelimishaji huu, tunalenga kuijengea jamii uelewa kuhusu athari zinazoweza kusababishwa na matumizi ya viatu virefu, namna ya kuchagua viatu vinavyofaa na hatua za kuchukua ili kulinda afya ya miguu na mwili kwa ujumla. Lengo si kuzuia watu kuvaa viatu virefu, bali kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi yanayowezesha kuunganisha urembo, starehe na afya.

1.33 MB
View Details
PDF

CHANZO CHA MIMBA KUTOKA MARA KWA MARA NA SULUHISHO LAKE

Kupoteza mimba mara kwa mara kunaweza kuleta huzuni, hofu na maswali kwa mwanamke na mwenzi wake. Hali hii inaweza kuwa na sababu mbalimbali, na wakati mwingine chanzo hakipatikani hata baada ya uchunguzi. Si kosa la mwanamke pekee. Ni muhimu wenzi kupata ushauri wa mtaalamu wa afya na kufanyiwa uchunguzi unaofaa kabla au wakati wa kupanga ujauzito mwingine. Takwimu zinaonyesha kuwa mimba kutoka ni changamoto muhimu ya afya ya uzazi. Nchini Tanzania, Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa mwaka 2022 uliripoti kuwa asilimia 8 ya mimba zilizotajwa na washiriki ziliishia kwa mimba kutoka. Katika Afrika Mashariki, utafiti uliochapishwa mwaka 2026 ulionyesha kuwa asilimia 14.8 ya wanawake walioshiriki waliripoti kupoteza ujauzito. Kwa kiwango cha dunia, uchambuzi wa tafiti za kisayansi uliochapishwa katika jarida la The Lancet mwaka 2021 ulikadiria kuwa mimba milioni 23 hutoka kila mwaka, huku takribani asilimia 15.3 ya mimba zinazotambuliwa zikiishia kwa mimba kutoka. Utafiti huo pia ulibaini kuwa kila dakika moja, mimba za wanawake 44 hutoka. Takwimu hizi zinaonesha umuhimu wa kuongeza elimu kuhusu afya ya uzazi, kuondoa unyanyapaa na kuwahimiza wanawake kupata ushauri wa kitaalamu wanapokumbana na changamoto hii.

279.19 KB
View Details
PDF

TAHADHARI JUU YA UGONJWA WA EBOLA

Ugonjwa wa Ebola ni ugonjwa hatari sana, tuchukue tahadhari. Na hizi ndizo dalili za Ebola na hatua za tahadhari za kufuata. Nenda kituo chochote cha affya pindi usikiapo/kuona mojawapo ya dalili hizi.

View Details
PDF

Matumizi sahihi na umuhimu wa mto wakati wa kulala.

Je, Ni Sahihi Kutumia Mto Wakati wa Kulala? Kutumia mto wakati wa kulala ni sahihi na kunaweza kusaidia kuweka kichwa, shingo na mgongo katika mkao unaofaa. Hata hivyo, hakuna mto mmoja unaofaa kila mtu. Muhimu ni kuchagua mto unaolingana na mkao wako wa kulala na unaokupa faraja. Kwa wanaolala chali, mto wenye unene wa wastani unaweza kusaidia shingo na kichwa kukaa vizuri. Kuweka mto mdogo chini ya magoti kunaweza kupunguza msongo kwenye sehemu ya chini ya mgongo. Kwa wanaolala ubavu, mto unapaswa kuwa na unene unaojaza nafasi kati ya kichwa na godoro ili shingo ibaki katika mkao wa kawaida. Mto mwembamba au mnene kupita kiasi unaweza kusababisha mkao usiofaa. Kwa wanaolala kifudifudi, mkao huu unaweza kulazimisha shingo kugeuzwa upande mmoja kwa muda mrefu, hivyo kuchangia maumivu ya shingo na mgongo. Ikiwezekana, ni vizuri kuzoea kulala chali au ubavu. Chagua mto kwa kuzingatia ukubwa, ugumu na faraja, huku ukihakikisha godoro linaunga mkono mwili vizuri. Ukiamka mara kwa mara na maumivu ya shingo au mgongo, kagua mkao wako na aina ya mto unaotumia. Ikiwa maumivu yanaendelea, yanaongezeka, au yanaambatana na ganzi au udhaifu wa mikono au miguu, muone mtaalamu wa afya. Hitimisho: Ubora wa usingizi hutegemea pia mkao wa kulala na msaada unaotolewa na mto na godoro. Chagua mto unaokufaa badala ya kufuata kanuni kwamba kila mtu lazima alale na mto au bila mto. Joseph Kisima, PT — Rally Polyclinic

1.09 MB
View Details
PDF

Je, Maumivu ya Mgongo au Kiuno Hupona Kabisa? Can back pain or lower back pain be completely cured?

“Mgongo wangu umekuwa ukiniuma kwa muda mrefu. Nimetumia dawa mbalimbali na mazoezi, lakini baada ya muda maumivu yanarudi. Je, kweli maumivu ya mgongo au kiuno yanaweza kuisha kabisa?” Hili ni swali linaloulizwa na watu wengi. Maumivu ya mgongo au kiuno ni tatizo linaloweza kumpata mtu wa umri wowote. Wakati mwingine huanza baada ya kufanya kazi nzito, kunyanyua kitu/vitu vizito, kukaa muda mrefu au kufanya shughuli zisizozoeleka. Kwa wengine, maumivu yanaweza kuendelea kwa muda mrefu na kuathiri kazi, usingizi na shughuli za kila siku. Habari njema ni kwamba maumivu mengi ya mgongo na kiuno yanaweza kutibiwa na kudhibitiwa vizuri, na watu wengi hurudi katika shughuli zao za kawaida. Hata hivyo, si kila maumivu yana sababu moja, na si kila mtu anaweza kupata suluhisho kwa kutumia njia ileile.

View Details
PDF

Je, Fiziotherapi ni Mazoezi, Mazoezi Tiba, au Huduma Jumuishi ya Matibabu? Is physiotherapy simply exercise, therapeutic exercise, or a comprehensive healthcare service?

DHANA ISIYO YA KWELI: “Fiziotherapi ni mazoezi ya mwili. Mtu anaweza kufanya mwenyewe nyumbani bila kuhitaji mtaalamu wa fiziotherapi!” UKWELI: Fiziotherapi si mazoezi ya kawaida tu. Ni huduma ya kitaalamu ya afya inayolenga kumsaidia mtu kurejesha, kuboresha au kudumisha uwezo wa mwili wa kufanya kazi na kushiriki katika shughuli za kila siku. Fiziotherapi huhusisha tathmini ya hali ya mgonjwa, kubaini changamoto zinazohusiana na maumivu, mjongeo wa mwili, nguvu za misuli, usawa wa mwili, uwezo wa kutembea na utendaji wa mwili, kisha kupanga na kutoa huduma inayofaa kulingana na mahitaji ya mgonjwa

View Details
PDF

Fiziotherapi ni nini na ina umuhimu gani kwa jamii? What is physiotherapy, and why is it important to the community?

Fiziotherapia (Physiotherapy) ni taaluma ya afya inayosaidia watu kurejesha, kuboresha na kudumisha uwezo wa mwili wa kufanya shughuli za kila siku. Mtaalamu wa fiziotherapi, anayejulikana kama Mfiziotherapia (physiotherapist), hutumia njia mbalimbali za kutambua tatizo la mgonjwa kama vile: Kuchukua taarifa za mgonjwa kwa njia ya mahojiano na mgonjwa au ndugu wa mgonjwa (history taking), uchunguzi kwa vitendo (physical examination), kupitia vipimo vya maabara (laboratory investigation), kumbukumbu za dawa (medication history), kupitia vipimo vya picha (radiological investigation) kama vile X – ray, CT – scan, MRI – scan, pamoja na kupitia kumbukumbu za nyuma za wataalamu wengine waliowahi kumhudumia mgonjwa kama zinapatikana (past medical history).

View Details

My Cart

Your cart is empty

 

 

Resolving Details