Je, Maumivu ya Mgongo au Kiuno Hupona Kabisa? Can back pain or lower back pain be completely cured?

PDF

Resource Details

“Mgongo wangu umekuwa ukiniuma kwa muda mrefu. Nimetumia dawa mbalimbali na mazoezi, lakini baada ya muda maumivu yanarudi. Je, kweli maumivu ya mgongo au kiuno yanaweza kuisha kabisa?”
Hili ni swali linaloulizwa na watu wengi. Maumivu ya mgongo au kiuno ni tatizo linaloweza kumpata mtu wa umri wowote. Wakati mwingine huanza baada ya kufanya kazi nzito, kunyanyua kitu/vitu vizito, kukaa muda mrefu au kufanya shughuli zisizozoeleka.
Kwa wengine, maumivu yanaweza kuendelea kwa muda mrefu na kuathiri kazi, usingizi na shughuli za kila siku.
Habari njema ni kwamba maumivu mengi ya mgongo na kiuno yanaweza kutibiwa na kudhibitiwa vizuri, na watu wengi hurudi katika shughuli zao za kawaida. Hata hivyo, si kila maumivu yana sababu moja, na si kila mtu anaweza kupata suluhisho kwa kutumia njia ileile.

My Cart

Your cart is empty

 

 

Resolving Details